Tuesday 17 April 2018

Mwanamke afungwa kwa kutaka kuunganisha Somalia na Somaliland



Mahakama ya Serikali imemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela mwanamke(Nacima Qorane) anayeimba mashairi kwa kosa la kuhamasisha Somaliland kuungana na Somalia

Mwanamke huyo amepatikana na makosa ya kuitukana nchi yake na kutokuwa mzalendo wa Serikali yake ya Somaliland

Bi.Qorane alikamatwa mwezi Januari akirejea kutoka Mogadishu, mji mkuu wa Somalia aliposema ametoka kuimba shairi la kuhamasisha umoja wa Somalia

Makundi ya wanaharakati nchini Somaliland wamesema Bi. Nacima Qorane ameminywa haki zake za kibinadamu

Somaliland ilijitambulisha kuwa huru mwaka 1991 licha ya kuwa taifa hilo halitambuliwi kimataifa

0 comments:

Post a Comment