Monday 23 April 2018

Nadal aonyesha ubabe mashindano ya tenis Japan


Rafael Nadal wa Hispania ameshinda ubingwa wa tennis wa michuano ya monte carlo masters ya nchini Ufaransa baada ya kumfunga Kei Nishikori wa Japan kwenye mechi ya fainali iliyopigwa jana mjini Monaco.
Nadal ambaye ni namba moja kwa viwango vya ubora wa mchezo huo kwa sasa duniani alimshinda Nishikori kwa seti ya 6-3 6-2.
Nako kwenye michuano ya kufuzu mashindano ya dunia, timu ya taifa ya Uingereza ya wanawake jana imefungwa na Japan kwa 3-2.
Uingereza iliyokuwa inaundwa na Johanna Konta pamoja na Heather Watson ilifungwa kwa seti ya 3-6 3-3 6-3 na timu ya japan iliyoundwa na Miyu Kato na Makoto Ninomiya.

0 comments:

Post a Comment