Monday, 23 April 2018

Mohamed Salah wa Misri atangazwa kuwa mchezaji bora kati ya wachezaji wa kulipwa wa ligi kuu nchini Uingereza


Mchezaji wa timu ya Liverpool Mohamed Salah kutoka Misri ameshinda taji la mchezaji bora kati ya wachezaji wa kulipwa katika ligi kuu ya nchini Uingereza kwa msimu wa 2017-2018 baada ya kupigiwa kura na wanachama wa chama cha wachezaji wa kulipwa PFA.
Salah ambaye msimu huu amecheza mechi 46 za mashindano tofauti na kufunga magoli 41, amewashinda wenzake Kevin De Bruyne wa Machester City na Harry Kane wa Tottenham.
Katika ligi kuu pekee, Salah amefunga magoli 31 na kuisaidia Liverpool kusalia katika nafasi za juu katika kipindi chote cha msimu huu, jambo linalomfanya sasa awe katika nafasi nzuri ya kushinda tuzo ya mfungaji bora na tuzo ya mchezaji kwa msimu huu.
Salah pia amejumishwa katika kikosi bora cha wachezaji 11 wa ligi kuu msimu huu kilichotajwa jana katika tuzo hizo.

0 comments:

Post a Comment