Friday 13 April 2018

Seneta Marekani adhihaki kiswahili akimhoji mmiliki wa Facebook




 Seneta John Kennedy atumia 'Kiswahili' kama fumbo la kumaanisha maandishi yasiyoeleweka wakati alipokuwa akimhoji Mmiliki wa Facebook, Mark Zuckerburg

  • Seneta huyo alikuwa akimhoji Zuckerburg katika bunge la Marekani juu ya sakata la matumizi mabaya ya taarifa za watumiaji wa mtandao huo

    Seneta Kennedy alimwambia Zuckerburg kuwa makubaliano yake na wateja(User Agreement) ni ya hovyo yanatakiwa yaandikwe kwa lugha inayoeleweka zaidi si iliyopo sasa aliyoifananisha na 'Kiswahili' ili ieleweke na watumiaji wa Amerika

    Alisema "Ninachoshauri nenda nyumbani kisha andika upya user agreement yako na mwambie mwanasheria wako unayemlipa $1200 kwa saa kuwa unataka iandikwe kwa 'Kiingereza na sio kwa Kiswahili' ili kila Mmarekani wa kawaida aweze kusoma na kuelewa."

    Seneta Kennedy, akihojiwa kuhusu kauli yake isiyofurahisha watumiaji wa Kiswahili duniani alisema "Sidhani kama kuna cha kuombea msamaha. Naamini kila mtu ameelewa nilichokuwa nakilenga"

0 comments:

Post a Comment