Wednesday 11 April 2018

Tyson hajavutiwa na Anthony Joshua


Bondia mkongwe duniani kutoka nchini Marekani, Mike Tyson amesema kwamba hajafuraishwa na kiwango cha bondia Anthony Joshua kutoka nchini Uingeleza katika pambano lake la mwisho, Tyson alisema hayo mara baada ya Anthony Joshua kuwa bingwa wa WBO, IBF na WBA.
“Joshua looked like he was the guy to (become undisputed champion) but in his last fight, he did not impress me,” Tyson aliiambia metro reports.

Joshua katika pambano lake la mwisho alishinda kwa points mara baada ya round 12 kuisha dhidi ya Joseph Parker. Anthony Joshua mpaka sasa hajapoteza pambano lolote kati ya mapambano 21 aliyopigana.

Mpaka sasa Anthony Joshua mkanda ambao hajachukua ni wa WBC ambao ataupigia dhidi ya bondia Deontay Wilder kutoka nchini Marekani. Deontay Wilder kapigana mapambano 39 na hajapoteza hata moja.
.

0 comments:

Post a Comment