Sunday 22 April 2018

Wabakaji kunyongwa nchini India



Serikali imeidhinisha hukumu ya kifo kwa watakaopatikana na hatia ya kuwabaka watoto wa umri wa chini ya miaka 12

Baraza la Mawaziri wa Serikali ya Waziri Mkuu Narendra Modi limepitisha amri hiyo na kuiwasilisha kwa Rais ili aiidhinishe

Bunge la nchi hiyo litahitajika kuiidhinisha katika kipindi cha miezi sita ijayo amri hiyo ili iwe sheria. Lakini kwa sasa washukiwa wanaweza kushtakiwa chini ya amri hiyo

Hatua hii imejiri baada ya kisa kilichozusha ghadhabu hivi karibuni cha msichana mwenye umri wa miaka minane kubakwa na kuuawa katika jimbo la Jammu-Kashmir, pamoja na visa vingine kama hivyo

0 comments:

Post a Comment