Tuesday 24 April 2018

Wivu wa mapenzi wawafanya wakatane mapanga



Mtu mmoja amefariki na wengine wawili kujeruhiwa vibaya katika kijiji cha Kingongo wilayani Serengeti kwa kukatana mapanga kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi

Marehemu ni Kibure Samwel(39) aliyechomwa kisu tumboni na kifuani. Majeruhi ni Nyanga'anyi Waitara(44), aliyejeruhiwa mkononi na Munge Samwel(44) aliyejeruhiwa pajani

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndani alisema chanzo cha ugomvi huo ni wivu wa mapenzi ambapo mwanamke (jina limehifadhiwa) alikuwa mke wa Waitara na sasa ameolewa na Munge

Alisema tangu mwanamke huyo aolewe na Munge kumekuwa na mgogoro baina yao na siku ya tukio walianza kutoleana maneno makali na baadaye kuanza kupigana kwa kutumia mapanga

Aliyefariki ni mdogo wa Munge ambaye alipofika kwenye tukio alimkuta kaka yake anashambuliwa na Waitara, hivyo akaamua kuchukua panga ili kumsaidia kaka yake lakini Waitara alimuwahi na kumchoma kisu tumboni na kifuani

0 comments:

Post a Comment