Wednesday 16 May 2018

Amber Rose amkumbuka 21 Savage



Baada ya kuwa na fununu kuachana lakini Amber Rose bado anampenda 21 Savage na haogopi kuonesha

“Nampenda sana huyu mwanaume” Amber Rose ameandika Instagram “Najua mitandao inanionesha kama mtu nisiye na moyo au siwezi kupenda lakini nampenda sana. Sio tu mmoja ya watu wenye vipaji niliowahi kukutana nao lakini ni mkweli, mnyenyekevu na akili sana”

Amber Rose hakuishia hapo aliongeza kwa kumshukuru rapper huyo wa “Bank Account” kwa jinsi alivyomjali yeye na mtoto wake, Sebastian pia na yeye amesema anawapenda watoto wa rapper huyo.

Mwezi wa tatu mwaka huu Amber Rose alithibitisha kuachana na 21 Savage lakini alidai kuwa hatafuti mtu mwingine kwani bado anampenda sana.

0 comments:

Post a Comment