Wednesday 16 May 2018

Kenyatta kaidhinisha sheria za mtandao Kenya



 Rais Uhuru Kenyatta ameidhinisha Muswada wa Sheria za Uhalifu wa Mtandaoni wa 2018 kuwa Sheria, sheria ambayo inatoa adhabu kali kwa watakaopatikana na makosa

Sheria hiyo inatoa adhabu kali kwa atakayepatikana na kosa la uenezaji wa habari za uzushi mtandaoni ya faini isiyozidi USD 50,000(Zaidi ya Tsh. Milioni 114) au kifungo hadi miaka miwili au vyote kwa pamoja

Aidha, mtu atakayepatikana na kosa la kueneza taarifa ambazo zinaweza kuzua taharuki au kuzua vurugu atafungwa jela zaidi ya miaka 10

Sheria hiyo pia inajumuisha adhabu kali kwa wale wote ambao watahusika kusambaza video za ngono za watoto

Sheria hiyo inatazamiwa kuathiri utendakazi wa wanahabari, vyombo vya habari, watumiaji wa mitandao ya kijamii, wanablogu na watu wengine wanaotumia kompyuta na mitandao

Wadau mbalimbali wa habari likiwemo Shirika la kimataifa la kutetea uhuru wa wanahabari Committee to Protect Journalists(CPJ) walikiwa wanamsihi Rais Kenyatta kutoidhinisha mswada wa sheria hiyo kuwa sheria

0 comments:

Post a Comment