Friday 4 May 2018

China na Korea Kaskazini wakutana


Kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong-un jana alikutana na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi mjini Pyongyang.
Bw. Wang Yi amesema China inawapongeza viongozi wa Korea Kaskazini na Korea Kusini kufanya mazungumzo na kutoa Azimio la Panmunjom. Amesema mazungumzo hayo yanatoa fursa ya kutatua suala la peninsula ya Korea kwa njia ya kisiasa.
Amesema China inaunga mkono kukomeshwa kwa hali ya vita kwenye Peninsula ya Korea, kuunga mkono Korea Kaskazini kubadilisha kipaumbele cha kimkakati kuwa ujenzi wa uchumi, na kushughulikia ufuatiliaji wake wa usalama wakati inaposukuma mbele mchakato wa kutimiza Peninsula ya Korea kutokuwa na silaha za nyuklia..
Bw. Kim Jong-un amesema kutimiza peninsula ya Korea kutokuwa na silaha za nyuklia ni msimamo thabiti wa Korea Kaskazini. Mabadiliko mazuri ya hali ya peninsula ya Korea ya hivi karibuni yana umuhimu mkubwa na yanasaidia kutatua suala hilo kwa amani.

0 comments:

Post a Comment