Jana ikiwa ni siku ya habari duniani, Shirika la kutetea haki za
wanahabari Press Emblem Campaign PEC limesema idadi ya wanahabari
waliouawa katika miezi minne ya mwanzo mwaka huu imefikia 44 katika nchi
18, ikiwa ni ongezeko la asilimia 57 kuliko mwaka jana kipindi kama
hicho.
Kwenye taarifa yake, PEC inalaani kuongezeka kwa wanahabari wahanga
wakati dunia inaadhimisha Siku ya uhuru wa vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa PEC, nchi zenye hatari kubwa zaidi kwa wanahabari tangu
mwanzoni mwa mwaka huu ni Afghanistan, Mexico, Syria, Ecuador, India na
Yemen
0 comments:
Post a Comment