Thursday 10 May 2018

Chris Brown katika tuhuma nzito za ubakaji



Chris Brown ameshtakiwa na mwanamke mmoja anayedai kuwa alibakwa na mwanaume na mwanamke ndani ya jumba la staa huyo wa R&B

TMZ wameripoti kuwa mwanamke huyo ambaye anajulikana kwa jina la Jane Doe amedai kuwa alialikwa kwenye House party ya Chris Brown mwezi february mwaka jana, alipofika hakuruhusiwa na watu wa Breezy kuingia na simu (huo ndio huwa utaratibu wa Chris Brown) lakini ndani alipewa kila kitu ikiwemo dawa za kulevya na bangi -

Baada ya muda, Jane Doe amedai kuwa mwanamke mmoja (hamfahamu) alimlazimisha pamoja na wanawake wengine ambao walikuwa wamealikwa kwenye hiyo party kufanya mapenzi na Brown baada ya kuufunga mlango na kuuzuia na kochi ili kuwazuia wasiondoke -

Amedai kuwa alipojaribu kuondoka yule mwanamke aliyewalazimisha kufanya mapenzi na Breezy, alimzuia akamlazimisha afanye mapenzi kwa njia ya mdomo na rafiki yake mwingine Chris Brown baada ya hapo huyo mwanamke akamlazimisha amfanyie na yeye mapenzi kwa mdomo (anadai huyo mwanamke alikuwa kwenye siku zake) -

Anasema baada ya hayo matukio aliamua kwenda kuoga ambapo rafiki yake Chris Brown mwingine (amemtaja kwa jina la Lowell Grissom) alienda akambaka, Jane amesema wakati anasubiri usafiri aondoke Grissom alimbaka tena. -

Amesema alivofanikiwa kuondoka alienda kwenye kituo cha matibabu ya wahanga wa ubakaji kuripoti ambao waliifikisha mashataka yake Polisi.
-
Mwanamke huyo anataka alipwe $ Million 17, Mwanasheria wa Chris Brown amekanusha shutma hizo.

0 comments:

Post a Comment