Thursday 10 May 2018

Simba mabingwa VPL



Klabu ya Soka Simba leo hii imetawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Bara, VPL 2017/18 baada ya Watani wao wa jadi Yanga kugaragazwa kwa kipogo cha goli 2-0 kutoka kwa Tanzania Prisons.

Katika mchezo wa Prisons na Yanga uliomalizika hivi punde magoli ya Prisons yamefungwa na Eliuter Mpepo(58') na la pili likifungwa na Salum Bosco(85')
 
Matokeo hayo ya Yanga iliyobaki na alama zake 48 inamaanisha wakishinda mechi zao 5 zilizobaki watafikisha alama 63 tu wakati Simba wana alama 65 mpaka sasa

0 comments:

Post a Comment