Mcheza tennis namba moja kwa
ubora kwa wanawake nchini Uingereza na namba 24 duniani, Johanna Konta
jana ameondolewa kwenye mashindano ya Hispania, Madrid Open baada ya
kufungwa na Bernarda Pera wa Marekani kwa seti ya alama 6-4 6-3.
Tangu mwaka huu uanze, Konta hajafuzu robo fainali ya michuano yote aliyoshiriki, na kwa kushindwa tena jana ilikuwa ni mara ya pili kufungwa na Pera ambaye ni namba 97 kwa ubora, kwani ndiye aliyemuondoa kwenye mashindano ya Australia mwanzoni mwezi machi.
Lakini kwa ushindi wa jana, Pera atakutana Carla Navarro Suarez wa Hispania kwenye raundi ya 3.

0 comments:
Post a Comment