Wednesday 9 May 2018

King Lebron James aipaisha timu yake katika hatua ya 'Conference Finals'


Mchezaji wa kimataifa wa mpira wa kikapu wa Marekani  Lebron James amepongezwa na mashabiki wa mchezo huo kutoka kila kona duniani kwa kuiwezesha timu ya mji wa nyumbani kwao ya Cleveland Cavaliers kufuzu hatua ya fainali ngazi ya kanda ya mashariki ya ligi ya kikapu nchini Marekani NBA.
Katika mechi ya nne kati ya saba za nusu fainali ngazi ya kanda ya mashariki iliyofanyika jana, Cavaliers walipata ushindi wa pointi 128-93, ukiwa ni ushindi wa nne mfululizo, na Lebron mwenyewe akifunga 29 katika mchezo huo.
Katika mechi ya fainali, Cleveland sasa watakutana na mshindi wa nusu fainali nyingine kwenye kanda hiyo kati ya Boston Celtics na Philadelphia 76ers.

0 comments:

Post a Comment