Wednesday 2 May 2018

Mahakama yamwondoa waziri mkuu Gabon



Huko nchini Gabon Mahakama ya Katiba yamuamuru Waziri Mkuu wa Nchi hiyo, Emmanuel Issoze-Ngondet kuondoka madarakani

Aidha Mahakama pia imetoa amri ya kuvunjwa kwa Bunge dogo la nchi hiyo kutokana na kuchelewa kwa Uchaguzi uliooadwa kufanyika mwisho wa wiki iliyopita

Mahakama imefikia uamuzi huo kwa maelezo kuwa muda wa Waziri Mkuu huyo pamoja na Wabunge umekwisha hivyo hawapaswi kuendelea kushika nafasi hizo

Mahakama imemtaka Rais Ali Bongo kkumteua Waziri Mkuu wa mpito atakayeongoza hadi uchaguzi utakapofanyika

0 comments:

Post a Comment