Wednesday 2 May 2018

Mei mosi yawa neema kwa wafanyakazi Kenya



Serikali ya Kenya yatangaza ongezeko la asilimia 5 kwa kima cha chini cha mshahara ili kuwalinda wafanyakazi na mfumuko wa bei uliofikia 4.8% mwaka huu.

Ongezeko hilo limetangazwa leo Mei Mosi, 2018 na Waziri wa Ajira na Mafao ya Kijamii, Ukur Yattani akisoma hotuba ya Rais Kenyatta katika viwanja vya Uhuru Park katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani mwaka huu.

Pia Serikali imeona upotevu wa masaa ya uzalishaji yaliyofikia milioni 100 kutokana na migomo ambayo imeona ni mbaya kwa taifa linaloendelea kama Kenya na kuona umuhimu wa kufanya mdahalo wa kitaifa na wadau ili kumaliza tatizo hilo.

0 comments:

Post a Comment