Tuesday 1 May 2018

Shambulizi laua watu 25 Afganistan



Nchini Afganistan Takribani watu 25 pamoja na Wanahabari watano wamefariki huku watu wengine 45 wakijeruhiwa katika mashambulio mawili ya mabomu ya kujitoa muhanga asubuhi ya jana.
 
Shambulio la kwanza lilitokea mapema asubuhi katika mji wa Shashdarak ambapo Ubalozi wa Marekani na majengo ya Serikali ya nchi hiyo yanapatikana, hivyo kusababisha Wanahabari kukimbilia katika eneo la tukio

Shambulio la pili limetokea ambapo aliyejitoa muhanga alivalia na kuonekana kama Mwandishi wa habari wa picha katika eneo ulipotokea mlipuko wa kwanza, alisema Msemaji wa Polisi

Eneo yalipotokea mashambulio hayo ni karibu na Makao Makuu ya NATO nchini humo, Ubalozi wa Marekani, Majengo ya Serikali ya nchi hiyo ikijumuisha Ikulu na Makao makuu ya Usalama wa Taifa pamoja na Wizara ya Ulinzi

0 comments:

Post a Comment