Tuesday 1 May 2018

Anthony Joshua kutoa maamuzi juu ya pambano lake na Deontay Wilder


Bondia Anthony Joshua wa Uingereza anatarajia kutangaza uamuzi wake wa kupigana ama kutopigana na mpizani wake, Deontay Wilder wa Marekani ndani ya siku kumi zijazo.

Joshua ameamua hivyo ili kuipa nafasi timu ya Wilder kuthibitisha endapo iko tayari kutoa fedha za kumlipa yeye endapo atakubali kushiriki pambano hilo.

Awali timu ya Wilder iliahidi kuweka rehani mikanda yake mitatu ya ubingwa wa WBO, IBF na WBA pamoja pesa taslimu Dola za Kimarekani Milioni 50.
Lakini kwa mujibu wa promota wa Joshua, Eddie Hearn, juhudi za kukutana na uongozi wa Wilder ili kujadili zinagonga mwamba.

0 comments:

Post a Comment