Thursday 17 May 2018

Uingereza yatangaza kikosi kitakachoshiriki kombe la dunia



Kocha wa timu ya Taifa ya Soka ya Uingereza, Gareth Southgate ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kuanza Juni 14, 2018 nchini Urusi

Kikosi hicho ambacho wastani wake kwa wachezaji kuitwa kwenye timu ya Taifa ni 19 huku aliyeitwa mara nyingi ni Gary Cahill(58), kinawakosa wachezaji kama Golikipa Joe Hart na kiungo Jack Wilshere

Aidha, Wachezaji Adam Lallana, Jake Livermore, Tom Heaton, Lewis Cook na James Tarkowski wapo kwenye orodha ya wachezaji ambao wanaweza kuitwa muda wowote

0 comments:

Post a Comment