Thursday 17 May 2018

Tanzanite One kuilipa serikali fidia



Kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzanite One imekubali kuilipa Serikali fidia pamoja na kodi watakayokubaliana kutokana na dosari zilizojitokeza hapo awali na kuiletea Serikali hasara

Makubaliano hayo yametiwa saini na Mwenyekiti wa Kamati ya Madini iliyoundwa na Rais Magufuli, Prof. Palamagamba Kabudi na Mkurugenzi wa Tanzanite One Faisal Juma

Katika makubaliano hayo fidia inatakiwa kulipwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza italipwa kwa muda wa wiki mbili kuanzia leo na haitahusiana na kodi. Aidha kodi na tozo nyingine zitalipwa kama kawaida

Mkugenzi wa Tanzanite One, Faisal Juma amesema kampuni hiyo itafuata taratibu zote za sheria ya madini za mwaka 2010 kwa lengo la kuhakikisha rasilimali za madini zinawanufaisha Watanzania na kwamba uvunjifu wa Sheria uliofanywa awali hautajirudia tena

0 comments:

Post a Comment