Wednesday 23 May 2018

Wanaochelewa kulala hatarini kufa mapema- Utafiti

  • Watu wanaochelewa kulala wana uwezekano mkubwa wa kufa mapema kuliko wale wanaowahi kulala
  •  

    Msingi wa utafiti huo ni kwamba watu wanaolala muda mzuri na kuamka mapema wanaweza kuishi muda mrefu ukilinganisha na wale ambao wanachelewa kulala ambao wakati mwingine wanaamka mapema wakiwa na uchovu mwingi

    Matokeo ya utafiti huo yamechambua sampuli ya watu laki 5 wenye umri wa miaka 30 hadi 73 ambao walifuatiliwa tabia za ulalaji wao kwa zaidi ya miaka 6 na nusu

    Watafiti walibaini kuwa watu ambao walikuwa wanachelewa kulala walikuwa na hatari kwa asilimia 10 kufa mapema katika kipindi cha utafiti kuliko wale ambao wanalala mapema na kuamka mapema

0 comments:

Post a Comment