Wednesday 23 May 2018

Joto laua watu 65 Pakistan



Nchini Pakistan katika mki wa Karachi  Viwango vya juu vya joto vyaua takribani watu 65 katika kipindi cha siku 3 tu Jijini humo.

Joto lilifikia nyuzijoto 44 siku ya Jumatatu ambacho ni kiwango kikubwa zaidi ya kiwango cha wastani vya joto kwa mwezi Mei cha nyuzi 35.

Matukio hayo ya vifo yanaaminika kuchochewa zaidi na kukatika kwa umeme katika jiji hilo hususan kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani kwa Waislamu.

Taarifa za vifo hivyo zilizotolewa na Shirika la huduma za kijamii la Edhi ambalo linaendesha Mochwari za Karachi zilipingwa vikali na mamlaka ya kudhibiti majanga ya jiji hilo wakidai ni madaktari tu wanaweza kuthibitisha vifo hivyo vimetokana na joto na wao wanajua ni mtu mmoja tu amefariki kwa sababu hiyo.

Hii si mara ya kwanza kwa hali hii kuipata Karachi. Mwaka 2015 joto lilifikia nyuzijoto 45 na kuua takribani watu 1300 wengi wakiwa wazee na wagonjwa.

Joto linatabiriwa kubaki juu ya nyuzijoto 40 kwa siku chache zijazo na kushuka kidogo mwishoni mwa wiki.

0 comments:

Post a Comment