Monday 25 June 2018

Kanye West, Jay Z kusimama kortini



Hoja zitakazo wasimamisha Kanye West Pamoja na Jay Z mahakamani Kwa mujibu wa mtandao wa Pitchfork, umeripoti kuwa, Tidal imewekwa kikaangoni kwa kosa la kuwandanganya wateja wake kuwa, album ya Kanye West 'The Life Of Pablo' ya mwaka 2016 itapatikana EXCLUSIVE tu kwenye mtandao wao. Kauli ambayo ilipigiwa msumari na Kanye ambaye ali-tweet :- "Will never never never be on Apple. And it will never be for sale . . . You can only get it on Tidal."- ilisomeka tweet hiyo.

Licha ya maneno yote, wiki 6 baadae 'T.L.O.P' ilipatikana kwenye Apple Music kitu ambacho kilimkasirisha shabiki mmoja wa Kanye aitwaye Justin Baker-Rhett ambaye alitumia pesa yake ku-subscribe Tidal akiamini ndio mahala pekee ambapo ataipata album hiyo.

#KanyeWest aliwahi kuibuka na kujitetea kuwa, album iliyowekwa kwenye Apple Music sio halisi kwa sababu imefanyiwa marekebisho kadhaa na ina utofauti mdogo na ile iliyopo #Tidal, hoja ambayo imepigwa chini na Jaji Gregory Woods.

Shabiki huyo anawaburuza Kanye na Tidal ya Jay-Z kwa kile alichodai kuwa, anahisi kutapeliwa na kudanganywa na Kanye pamoja na Tidal.

Kwa mujibu wa Mwanasheria wake, amepanga kumshinda Kanye kwenye kesi hiyo: "We now will have a chance to move on with this case, including deposing Kanye," alisema Edelson.

0 comments:

Post a Comment