Tuesday 26 June 2018

Khaligraph apata baraka kutoka kwa mama yake



Rapa kutoka Kenya, Khaligraph Jones ameonekana akiwa Studio na mama yake mzazi na kilichoonekana zaidi ni Baraka na maombi ya mafanikio kwa mwanae huyo anayefanya vizuri na kolabo ya wimbo wake alioshirikiana na umoja wa wakali wawili, Roma na Stamina 'ROSTAM' kutoka Tanzania kwa jina 'Now You Know'.

Wakiwa Studio Khali alicheza wimbo mmoja ambao alisikika akichana na pale pale rapa huyo alifanya kufatiliza uchanaji wa mistari ya wimbo huo aliyorekodi jambo lililotengeneza Sura ya tabasamu kwa mama mzazi wa rapa huyo.

Kingine kilichovutia katika video hiyo ambayo Khaligraph aliiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram ni Mama huyo kuonekana kwenye mkono wake akiwa mashikilia mkebe wa album mpya ya Khaligraph Jones 'Testmony1990' na hii imeonesha kuwa Safari ya mafanikio ya Khali imejwa na Baraka tele za Mama.

0 comments:

Post a Comment