Tuesday 26 June 2018

Padri 'Rapa' asimamwishwa kazi



Kasisi (Padri) mmoja wa kanisa Katoliki nchini Kenya aliyepata umaarufu kutokana na mtindo wake wa kutumbuiza kwa kutumia muziki wa kufoka amesimamishwa kazi.

Paul Ogalo aka 'Sweet Paul' amekuwa akitumia muziki wa rap kama njia ya kuwavutia vijana wengi kufika kanisani.

Mistari ya nyimbo zake huwa kwa mfano: "Kujeni church kuna baraka, kujeni church kuna baraka..." au "Father Paul, niki-lock kwenye mic, Nduru inafuata, mamanze go tipsy, vijana ruka ruka swag ya kunguru, au sio" - Swipe kuona akichana kanisani.

Lakini hatua yake hiyo inaonekana kutowafurahisha viongozi wa kanisa Katoliki magharibi mwa Kenya ambao wamemsimamisha kazi kwa mwaka mmoja ili "ajitafakari".- Askofu wa jimbo la kanisa Katoliki la Homa Bay Philip Anyolo amesema padri huyo ni lazima achague kati ya kuwa rapa na kuwa padri.

0 comments:

Post a Comment