Friday 6 July 2018

Aishtaki kampuni ya Condom zisizokuwa na ubora



Mtu mmoja nchini Kenya amevishtaki vitengo vya serikali na kampuni za kuuza dawa kuhusu mpira wa kondomu uliopasuka na kumfanya kuambukizwa magonjwa.

Mlalamikaji huyo anataka kulipwa fidia kutoka kwa kampuni ya dawa ya Beta Healthcare Ltd kufuatia kisa hicho ambacho anasema kondomu hiyo ilipasuka alipokuwa akifanya mapenzi na mpango wake wa kando (mchepuko) swala lililosababisha ndoa yake kuvunjika.

Kwa mujibu wa Mwandishi wa BBC, jamaa huyo anadai kuwa aliitumia kondomu hiyo kufanya mapenzi na mwanamke aliyekutana naye kwenye harusi, lakini ikapasuka wakati wa tendo la ngono. Alipuuzia kisa hicho na siku tatu baadaye alikutana kimwili na mkewe kisha kumuambukiza Ugonjwa wa zinaa.

Mke aliamua kumkimbia jamaa na kwenda kwa mwanaume mwingine. Jamaa huyo sasa anaitaka kampuni ya Beta Healthcare Ltd kumlipa kwa dhiki na hasara ya kibinafsi aliyoipata wakati wa tendo hilo. Pia ameitaka serikali kuzipiga faini Mamlaka ya mapato KRA na Shirika la Ubora wa bidhaa KBS kwa kuruhusu bidhaa zisizofikia kiwango kuingia nchini.

0 comments:

Post a Comment