Wednesday 4 July 2018

Akutwa hai kwenye chumba cha kuhifadhia maiti



Mwanamke mmoja amelazwa katika hospitali ya Leratong baada ya kukutwa hai katika jokofu kwenye chumba cha kuhifadhia maiti

Mfanyakazi katika chumba hicho aligundua bado mwanamke huyo anapumua wakati alipofika kuutizama mwili na kutayarisha nyaraka kumhusu

Mwanamke huyo alifikishwa katika chumba hicho baada ya madaktari kusema amefariki kutokana na kutoonesha dalili zozote za uhai kufuatia ajali ya barabarani aliyoipata

Familia ya mwanamke huyo imesema wamepata mshtuko mkubwa na wana wasiwasi kuhusu mkasa huo hivyo wanahitaji ufafanuzi ni vipi makosa hayo yanaweza kutokea

0 comments:

Post a Comment