Tuesday 3 July 2018

Arsenal yanyakua saini ya kiungo Dortumund



Beki Sokratis Papastathopoulos amekamilisha usajili wa kujiunga na Klabu ya Arsenal akitokea Borusia Dortmund ya Ujerumani.

Beki huyo wa kati raia wa Ugiriki amejiunga na Arsenal kwa mkataba wa muda mrefu ambao kiwango chake cha fedha kimetajwa kuwa ni £17m, na kukabidhiwa jezi namba 5.

Sokratis 33' aliitumikia Borusia Dortmund tangu mwaka 2013 na alifanikiwa kushinda mataji mawili ya Bundesliga na taji moja la ligi 'German Cup' .

Huu ni usajili wa tatu kwa Kocha mpya wa Arsenal, Unai Emery ambaye alianza kwa kumsajili beki Stephan Lichtsteiner toka Juventus, Goli kipa Bernd Leno toka Buyern Leverkusen.

0 comments:

Post a Comment