Friday 20 July 2018

Liverpool na Becker, asaini miaka 6 Anfield


Klabu ya Liverpool imefanikiwa kumsajili kipa aliyekuwa akichezea AS Roma kwa mkataba wa miaka 6 kwa dau la Pauni milioni 67. Klabu hiyo imefikia makubaliano na mlinda mlango huyo ambaye alikuwa akiwaniwa na klabu zingine za Uingereza. Ujio wa Becker unawapa wakati mgumu Simon Mignolet na Karius kutokana na ubora mkubwa wa Becker ambaye ni kipa namba moja wa timu ya taifa ya Brazil

0 comments:

Post a Comment