Terrence Levarr Thornton maarufu kama Pusha T, ni raisi wa label ya GOOD MUSIC inayosimamia wasanii kama Desiigner, Big Sean, na Tayana Taylor, siku ya jana alifunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Virginia Williams katika Hotel maarufu ya Cavalier Hotel katika fukwe za Virginia.
Harusi hiyo ilihudhuriwa na mastaa kibao akiwemo Pharrel Williams ambae alikuwa best man wa Pusha T, pia alikuwepo Kanye West pamoja na mkewe Kim Kardashian. Baada ya kufunga ndoa Pusha T alichukua mic na kuanza kuburudisha wageni kwa mistari.
Mwaka huu Pusha T alitengeneza headlines nyingi mitandaoni baada ya kuachia album ya "Daytona" ambayo ilikua na diss track kwa Drake kupitia track ya "Infrared", na kupelekea Drake kumjibu kupitia ngoma ya "Duppy Freestyle", lakini Pusha T alimaliza utata wa Drake baada ya kumjibu kupitia "The Story Of Adidon" track ambayo ilifichua siri ya Drake kuwa na mtoto.
.
.
Blogged by @silverracca
0 comments:
Post a Comment