Wednesday 11 July 2018

Yemi Alade akataa kuwa chini ya Davido na Wizkid



Mwanadada kutoka nchini Nigeria, Yemi Alade amefunguka kuwa hakuna msanii mkubwa na namba moja kwa Nigeria, wote wapo sawa.. hakuna cha Wizkid wala Davido.

Yemi ameitoa kauli hiyo kwenye mahojiano na kituo cha redio cha Hot 93.7 FM, baada ya kuulizwa ni yupi msanii namba moja Nigeria kwa sasa? - alijibu
"Nina waheshimu wasanii wote, kiukweli hakuna msanii namba moja." Alisema Yemi Alade nakuendelea.

"Kiwango cha watu ambacho Wizkid anajaza kwa Afrika, hata mimi najaza, kiwango ambacho Davido anajaza pia mimi huwa najaza, viwanja hivyo hivyo. Wote tunajaza hivyo hakuna msanii namba moja na huo ndio ukweli, japo wengi watasema Yemi funga mdomo wako lakini huo ndio ukweli!."- alisema Yemi Alade.

0 comments:

Post a Comment