Friday 17 August 2018

Makampuni ya viatu ya wanamuziki washika namba moja kwa ushirikiano


YEEZY na Pharrell walioingia ushirikiano na Adidas pamoja na Rihanna 'FENTY' ambaye anaushirikiano na PUMA, ushirikiano huo wa wanamuziki umeonekana kufanya vizuri zaidi kwenye soko la mauzo ya viatu (Sneaker) kuliko wachezaji.

Kwa mujibu wa Stadium Goods, mauzo ya Kanye West, Pharrell na Rihanna yana thamani ya juu zaidi kuliko wacheza kikapu. Takwimu zinaeleza kuwa Kanye West ameuza 70.9% ya Sneaker zaidi ya Steph Curry na mauzo yake ya jumla ni 9.4% juu zaidi ya Lebron James.

Pharrell pia ametajwa kuuza mara mbili zaidi ya Lebron huku mauzo yao ya pamoja na Kanye yakifikia 80% zaidi ya viatu vya mastaa wengi wa kikapu akiwemo Paul George, Damien Lillard na Steph Curry kwa pamoja.

Wanamuziki wengi akiwemo Rihanna, Travis Scott na Drake pia wamefanya vizuri zaidi kwenye soko la mauzo kuliko wanamichezo.

Muanzilishi mwenza wa mtandao wa kuuza viatu mtandaoni wa Stadium Goods, Jed Still ametoa mawazo yake ya kwanini Wanamuziki wameweza kufanya vizuri zaidi. Amesema ushawishi mkubwa walionao wasanii kwenye jamii hasa kupitia mitandao yao ya kijamii umekuwa msaada mkubwa kwa mauzo hayo ukilinganisha na wachezaji.

Kwa habari za chini chini kuhusu viatu, rapper Travis Scott amedokeza juu ya ujio wa ushirikiano wake na kampuni ya Air Force 1.

0 comments:

Post a Comment