Tuesday 18 September 2018

Bondia Anthony Joshua asema hatodharau pambano la jumamosi


Bondia Anthony Joshua AJ wa Uingereza ametangaza kuwa kamwe hatadharau pambano lake la jumamosi dhidi ya Alexander 'Sasha' Povektin wa Urusi litakalopigwa jumamosi ijayo Septemba 22 katika uwanja wa Wembley mjini London.
Katika pamabano hilo, AJ anatarajiwa kutetea mikanda yake mitatu ya ubingwa wa WBO, IBF na WBA huku akiwa na shinikio kubwa la kulinda rekodi ya kutowahi kupigwa katika mapambano yote 21 aliyowahi kushiriki tangu aanze masumbwi.
Povektin mwenye rekodi ya kupoteza pambano moja tu kati ya 35 aliyowahi kushiriki amekutana na mpinzani wake kwenye mkutano wa kutambulisha pambano hilo jana.

0 comments:

Post a Comment