Wednesday 22 November 2017

Hali tete katika kuunda serikali ya muungano nchini Ujerumani


Rais wa shirikisho, Frank-Walter Steinmeier anaonana na viongozi wa FDP na die Grüne katika juhudi za kuyanusuru mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano baada ya mazungumzo hayo kuvunjika jumapili usiku.
 Leo rais wa shirikisho Frank-Walter Steinmeier atakutana kwa mazungumzo katika kasri la Bellevue kwanza na viongozi wa chama cha walinzi wa mazingira die Grüne  Simone Peter na Cem Özdemir na baadae na mwenyekiti wa chama cha kiliberali cha FDP, Christian Lindner. Alhamisi rais wa shirikisho atakutana na mwenyekiti wa chama cha Social Democrat, Martin Schulz.
Lengo la juhudi hizo ni kujaribu kuwatanabahisha viongozi hao umuhimu wa kuyanusuru mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano , baada ya mazungumzo hayo kuvunjika usiku wa manane wa jumapili kuamkia jumatatu ya jana. Hiyo hiyo jana rais wa shirikisho alikutana na kansela Angela Merkel na kuzungumzia baadae umuhimu kwa pande zote kutafakari misimamo yao na kuelezea shaka shaka zake kuelekea uchaguzi mpya.
Spoika wa bunge la shirikisho Wolfgang Schäuble

0 comments:

Post a Comment