Sunday 25 February 2018

Mgodi wa Buzwagi wafugwa



Zaidi ya wafanyakazi 1,300 wamekosa ajira, huku Kodi ya Sh. Bilioni 28 ikipotea baada ya Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi kufungwa rasmi.

Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa mgodi huo unaomilikiwa na Acacia, umefungwa baada ya kushindwa kuzaliwa kiwango cha madini ya dhahabu kilichotarajiwa

Uongozi wa mgodi huo umeeleza kuwa uzalishaji wa dhahabu katika eneo la mgodi umeshuka kutoka gramu 1.35 hadi 1.00 (kwa kila kilo moja ya mchanga/mawe inayochimbwa) kwa mwaka jana.
Tayari mgodi huo umeanza kuuza baadhi ya mali zake yakiwamo magari, mashine, majengo na vifaa vingine. Mnada mkubwa wa kuuza mali za mgodi huo utafanyika mapema mwezi Machi, 2018.

0 comments:

Post a Comment