Mbunge
wa Tarime Vijijini, John Heche amekiri bila busara za Spika wa Bunge
kutumika leo angekuwa amekamatwa leo na polisi wamedaiwa kutoka Morogoro
waliokuwa eneo la Bunge kwa nia ya kumkamata.
Mh. Heche amweka hilo wazi jioni hii huku akikosoa matumizi mabaya ya rasilimali iliyotumiwa.
"Nimepokea
barua ya polisi asubuhi leo wakinitaka kuripoti Morogoro eti kwa kosa
la kumsindikiza na kufanya mkutano jimboni kwa Mh Lijualikali alipotoka
gerezani mwezi wa 4" Amesema Heche na kuongeza;
"Kabla hata ya kuitikia wanataka kunikamata bila busara za spika wangenikata. Matumizi mabovu ya rasilimali"
Kabla ya taarifa hii kutoka Mapema leo Heche alikiri kupokea wito unaomtaka kwenda kuhojiwa Morogoro.
"Nimepewa
wito kuwa natakiwa nikahojiwe Morogoro. Nimepokea wito huu na tayari
nao wako hapa. Siamini kama Spika ataruhusu hili," amesema Heche.
0 comments:
Post a Comment