Wednesday 1 November 2017

JPM:Aunga Mkono Juhudi za Wananchi


Rais Dkt John Magufuli Jana katika ziara yake mkoani mwanza ameonekana kupendezwa na juhudi zinazofanywa na baadhi ya wananchi pia alitembelea viwanda tofauti jijini hapo.
Akiwa katika kiwanda cha saruji Rais Magufuli alitoa Sh milioni tatu kwa lengo la kununulia mifuko 100 ya saruji kwa shule mbili zilizopo ndani ya kata hiyo.

Rais Magufuli alimkabidhi fedha Diwani wa Kata ya Igogo, John Minja, akiunga mkono juhudi za wananchi wa kata hiyo katika kuboresha miundombinu.

Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula, alimweleza Rais Magufuli kuwa wananchi wa kata hiyo wamechanga Sh milioni 15.8 kujenga matundu ya vyoo, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuwa aliwahi kuishi ndani ya kata hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Kiwanda cha Victoria Moulders & Polybags, Manjist Singh, alisema bidhaa zinazozalishwa hapo zinauzwa Uganda, Rwanda, Burundi na ndani ya nchi na kuongeza kuwa alikianzisha kutokana na uwepo wa shughuli za kilimo na madini.

Hata hivyo, aliomba Serikali kupunguza matatizo yaliyopo soko la ndani kwa kuondoa utegemezi wa bidhaa za nje kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wawekezaji wa ndani.

0 comments:

Post a Comment