Wednesday 1 November 2017

Raia 2 wa Tanzania na 10 wa Iran wakamatwa kwa dawa za kulevya

Maboti yanayojulikana kama dhow huonekana katika pwani ya bahari ya Tanzania

Image caption
Raia 10 wa Iran na wawili wa Tanzania wameshtakiwa kwa kuingiza kinyume na sheria takriban kilo 100 za dawa za kulevya aina ya heroine kupitia bahari hindi kulingana na gazeti la The Citizen nchini tanzania.
Kulingana na gazeti hilo 12 hao walikamatwa wakiabiri boti kwa jina dhow lililobeba dawa hiyo katika pwani ya Zanzibar Jumanne iliopita wakati maafisa wa shirika la kukabiliana na mihadarati wakishirikiana na maafisa wa usalama walipokuwa wakipiga doria za vita dhidi ya dawa za kulevya.
Mahakama ya eneo la Kisutu iliambiwa kwamba washukiwa hao walikamatwa katika maji ya Tanzania mnamo tarehe 25 mwezi Novemba walipokuwa wakipenyeza kilo 111.2 za dawa ya heroine , iliochanganywa na bangi .
Hakimu wa mahakama hiyo alikataa ombi la washukiwa hao kuachiliwa kwa dhamana.

0 comments:

Post a Comment