Thursday, 16 November 2017

Mchoro ya Yesu wauzwa dola milioni 450 Marekani

Mchoro wa miaka 500 wa Yesu unaoaminiwa kuchorwa na Leonardo da Vinci, umeuzwa mjini New York kwa kima cha dola milioni 450.
Mchoro huo unajulikana kama Salvator Mundi (Mkombozi wa Dunia).
Ndio mchoro wa bei ya juu zaidi kuwai kuuzwa kwa mnada.

Leonardo da Vinci alifarika mwaka 1519 na kuna chini ya 20 ya michoro yake iliyobaki.
Ni huo mmoja tu unaoaminiwa kuwa mikononi mwa mtu ambao unaamimiwa kuwa ulichorwa baada ya mwaka 1505.


Picha hiyo inamuonyesh Yesu akiwa ameunua mkono mmoja huku mwingine ukishika kioo.
Mwaka 1958 mchoro huo uliuzwa kwenye soko la mnada mjini London kwa Dola 60. Wakati huo mchoro huo uliaminiwa kuwa kazi ya mfuasi wa Leonardo na wala haukuwa wa Leonardo mwenyewe

Miaka minne iliyopita mchoro huo ulinunuliwa na raia wa Urusi kwa dola milion 127.5 lakini wakati huo hakuuzwa katika mnada.

0 comments:

Post a Comment