Saturday 4 November 2017

Mchungaji Kutoka kwenye maji hadi kubatiza kwa pombe



Mchungaji mmoja kutoka nchini Afrika Kusini amekuwa gumzo hadi kupelekea kukoselewa  vikali baada ya kuanza kubatiza washirika kwa kutumia vilevi ambavyo wanavipenda kitendo ambacho ni cha udhaulilishaji kwa waumini wake na katika dhehebu la kikistro.
Askofu  huyo ajulikanaye kama Tsietsi Makiti, (52) ambaye pia  ni Mwanzilishi wa kanisa hilo linalojulikana kama 'Gabola', amesema kuwa ameongozwa na maandiko katika Biblia ambapo Yesu alibadilisha maji kuwa divai.

"Watu wanao kunywa na kubatizwa na bia wana furaha na amani. Hii inamaanisha kuwa wanaishi katika kivuli cha Mungu, "alisema Makiti.

Kanisa hilo lenye jina 'Gabola' jina likimaanisha 'Kunywa' limesema linakubali kuwapokea waumini waliotoka makanisa mengine huku likiweka wazi kwamba idadi ya watu wameongezeka kufikia 500 ndani ya miezi miwili tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo.
Kiongozi huyo wa kanisa la 'Gabola'awauhusu Waumini wake kutumia vilevi pindihuduma za kioho zikiwa zinaenelea kanisani.
Aidha Askofu huyo ameweka wazi kwamba ana mipango ya kuanzisha matawi ya kanisa lake hilo katika miji mbali mbali nchini humo.

0 comments:

Post a Comment