Monday 20 November 2017

Mugabe akataa kujiuzulu, huenda akaondolewa kisheria


Kiongozi wa muda mrefu nchini Zimbabwe, Rais Robert Mugabe anakabiliwa na mashtaka ya kutaka kumuondoa mamlakani baada ya kueleza dhahiri katika hotuba yake Jumapili kuwa hatajiuzulu
.
Mamilioni wa watu walisikiliza na kuangalia kwenye televisheni hotuba hiyo wakitarajia kusherehekea mwisho wa miaka 37 ya utawala wa Mugabe.
Wakiwa wamesikitishwa sana, baadhi yao walibubujikwa na machozi walipomsikia Mugabe akisema atashiriki katika mkutano mkuu wa ZANU-PF uliopangwa kufanyika mwezi ujao.
Hakuzungumzia suala la kujiuzulu au kutilia maanani hatua ya jeshi kuingilia kati na hivyo kusababisha mzozo wa kisiasa.
Mapema chama tawala cha ZANU-PF kilimwondoa Mugabe kama mkuu wa chama hicho ambacho alikianzisha pamoja na wagombea uhuru wengine na kumtaja makamu wa rais aliyeondolewa madarakani Emersong Mnangagwa ndiye kiongozi mpya wa chama.
Chama hicho kimempa Mugabe hadi Jumatatu mchana kuachia madaraka ama sivyo atafunguliwa mashitaka ya kumwondoa madarakani

0 comments:

Post a Comment