Saturday 4 November 2017

Q Boy Msafi: Mr Blue Alikosa muda kutokea kwenye video


Q Boy Msafi  akiongea na EATV kupitia kipindi cha enewz akiri kama  Mr. Blue angekataa kufanya kazi na yeye angeanza kwenye audio lakini alionyesha ushirikiano toka mwanzo na kutokuwepo kwenye video ni mwingiliano wa ratiba tu.
“Siyo kweli kwa sababu kama ni kunivimbia angeanza kwenye audio lakini kwenye audio, ingia usikie alichokifanya cha kwanza aliniimbia verse ambayo inaendana na wakati kwa sababu flow alizoendana nazo hadi watu wanasema Mr. Blue mbona kama kabadilika,”amesema.

“Kweli nawambia Mr. Blue hajanivimbia ila mwisho wa siku hii ni sanaa kila mtu anaweka mkakati wa kazi yake, asingeacha sehemu ambayo ina ugali ili kuniridhisha mimi, uzuri ni kwamba alinijuza,” ameongeza Q Boy.
Kamoyo ni ngoma ya tatu kwa Q Boy kutoa official mara baada ya mbili za mwanzo ambanzo ambazo ni Karorero na Unaanzaje.

0 comments:

Post a Comment