Tuesday 5 December 2017

Atetea taji lake la mtu mbaya kwa Mara ya tatu




William Masvinu mwenye miaka 43 ameshinda shindano la mtu mwenye sura mbaya nchini Zimbabwe. Masvinu alishinda kwa points 98 huku mpinzani wake Fanuel Musekiwa akishika nafasi ya pili kwa points 61.


Masvinu alikuwa mshindi mwaka 2012 na 2013 katika mashindano hayo ya watu wabaya. Baada ya kushinda taji hilo alisema,
"Mashindano yalikuwa magumu kwa sababu watu wote walikua wabaya hata mimi mwenyewe siamini kama nimeshinda shindano hili"


Pia Masvinu aliongeza
"Najivunia kuwa na sura mbaya na kuzaliwa mbaya sijawahi kujutia kuwa hivi najivunia sana sura yangu"


Mshindi wa shindano hilo alipata kiasi cha dollar 500 na mshindi wa pili dollar 200 huku watatu akipata dollar 100.

0 comments:

Post a Comment