Kenya imesema
kwamba itaendelea na mpango wake wa kuhakikisha kwamba ina kiwanda cha
kuzaliwa umeme kwa kutumia nguvu za nyuklia kufikia 2027.
Afisa
Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Umeme wa Nyuklia ya Kenya Collins Juma ameambia
mkutano wa wadau kuhusu kawi jijini Nairobi kwamba ujezi wa kiwanda cha
kuzalisha kawi hiyo unatarajiwa kuanza 2024.Bodi hiyo imesema nishati hiyo itatumiwa kuongeza uzalishaji wa umeme nchini humo na si kuchukua nafasi ambayo imekuwa ikitekelezwa na vyanzo vingine vya kawi nchini humo.
Kufikia mwaka 2030, ambapo Kenya inatazamia kuwa taifa lenye viwanda la mapato ya wastani kufikia wakati huo, Kenya itakuwa ikihitaji megawati 17,000.
Kawi ya mvuke itachangia megawati 7,000. Kwa sasa, kawi hiyo kwa sasa hutumiwa kuzaliwa megawati 2,400 za umeme nchini humo.
0 comments:
Post a Comment