Monday 18 December 2017

Chama cha ANC chaanza duru ya kumtafuta mwenyekiti atakae gombea urais 2019 Afrika kusini




Mkutano mkuu wa chama tawala nchini Afrika Kusini cha ANC, umeanza jana jumamosi jijini Johannesburg ukiwa na kauli mbiu inayohimiza umoja.
Mkutano huo unatarajiwa kumchagua rais wa chama hicho, mwenyekiti, katibu mkuu pamoja na viongozi wengine wa chama.
Makamu wa Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa na aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma wanawania kumrithi Jacob Zuma katika nafasi ya mwenyekiti wa chama na wakitarajiwa pia kugombea nafasi ya Urais wa kupitia chama hicho mwaka 2019.
Akihutubia mkutano huo, Zuma amehimiza umoja ndani ya chama huku akikiri kuwa jamii imekosa imani na mwenendo wa chama tawala kwa sasa na serikali kwa ujumla.
Pia Rais huyo amekiri kuwa uchumi wa nchi hiyo ni dhaifu kwa sasa, hivyo akahimiza kuwa mapambano yanahitajika dhidi ya umaskini, ukosefu wa usawa na tatizo la ajira.

0 comments:

Post a Comment