Bandari kavu ya kontena ya Nairobi ni mradi muhimu unaoambatana na reli ya kisasa ya SGR ya Mombasa-Nairobi, iliyoanza safari tarehe 31, Mei mwaka huu. Reli hiyo ilijengwa na kampuni ya ujenzi wa barabara na madaraja ya China CRBC. Hivi sasa ujenzi wa awamu ya kwanza wa reli ya Nairobi-Malaba ambayo ni ya kurefusha reli ya Nairobi-Mombasa umeanza.
Akiwa kwenye sherehe hizo, rais Kenyatta amesema bandari kavu ya kontena ni juhudi za hali ya juu za kuinua usafirishaji wa bidhaa na uwezo wa usimamizi wa Kenya na hata kanda ya Afrika Mashariki. Anasema,
"Reli ya Nairobi-Malaba itapita katika bandari hiyo kavu ya kontena, na baadaye kuunganisha Nairobi na maeneo yaliyo kando ya reli hiyo. Kwa mujibu wa ustawi wa kikanda, reli ya uchukuzi ya SGR itapunguza gharama za kibiashara za kanda nzima ya Afrika Mashariki. Kwa hivyo, narudia tena shukrani zangu kwa mwenzi wetu wa ushirikiano, Jamhuri ya Watu wa China kutokana na uungaji mkono wao thabiti"
Naye kaimu balozi wa China nchini Kenya Li Xuhang amesema tangu kuzinduliwa nusu mwaka uliopita, reli ya Maomba-Nairobi imebeba abiria laki 6, na kuzinduliwa kwa bandari kavu ya kontena ya Nairobi na uchukuzi wa kibiashara kutakuwa jambo jipya lenye kihistoria katika ujenzi wa reli ya Mombasa-Nairobi, na pia ni matokeo mapya ya ushirikiano kati ya China na Kenya mwaka 2017.
0 comments:
Post a Comment