Mwanamuziki na mwanamitindo maarufu nchi Jokate mwegelo amewataka vijana kujua faida za mitandao ya kijamii na kuacha kupoteza muda kufatilia vitu visivyowaletea maendeleo ameyasema hayo kupitia radio ya East Africa.
Jokate
ambaye ni mjasiliamali pamoja na mhamasishaji haswa kwa vijana, kwa
sasa yupo katika kampeni ya kuwakumbusha vijana wajibu wao ili waweze
kujitambua kupitia kampuni ya Sahara Group inayo saidia kuwapa Elimu
vijana juu ya mustakabali wamaisha yao. ''Vijana wasitumie mitandao ya kijamii kujua kuwa Jokate
amevaaje leo, au kaweka nywele gani , inatakiwa watafute taarifa
mbalimbali ambazo kila wakati hutolewa katika 'Internet' ili ziweze
kuwapa ufahamu na pengine kuwasaidia, "Ni vizuri kijana kuwa na kazi yake akijiamulia mwenyewe kwamba leo afanye kazi gani na afanye nini anakuwa huru sana,'' amesema
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa njia sahihi ya elimu kwa vijana juu
ya kujitegemea ianzie vyuoni ili wakati wanapomaliza wanakuwa tayari
wameweza kujua njia sahihi ya kuji kwamua.
0 comments:
Post a Comment