Mwanasheria msomi na mbunge wa Singida mashariki kupitia tiketi ya Chadema Tundu Lissu, hatimaye ameanza kusimama kwa mara ya kwanza baada ya kushambuliwa jijini Dodoma mwezi septemba.
Tundu Lissu amekuwa akipokea matibabu nchini Kenya tangu alipopigwa risasi na watu wasiojulikana .Leo kupitia ukurasa wa Facebook wa CHADEMA, mbunge huyo anaonekena akisimama huku akisaidiwa na wahudumu wawili wa hospitali.
Ujumbe ulioambatana na picha ukisema "Wiki iliyopita niliwataarifu kwamba madaktari wangu wamesema 'nitasimama, nitatembea na nitarudi Tanzania.Leo Boxing Day (Tarehe 26 Disemba) nimeweza kusimama kwa mguu mmoja kwa msaada wa 'Mababa Cheza' wangu. Hatua inayofuata ni magongo kesho na nitawajulisheni hatua nyingine katika matibabu yangu."
0 comments:
Post a Comment