Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF), Maulid Said Abdallah Mtulia amewataka wananchi wa wilaya ya Kinondoni kuchagua Mbunge wa Chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi ujao ili kuharakisha maendeleo katika jimbo.
“Naamini Kama ningekuwa Mbunge wa Chama tawala ningeweza kutekeleza vizuri zaidi ahadi zangu ambazo nimezitoa kwa wananchi wangu.. Kwa sababu hiyo nimeona sasa ni bora nijivue nafasi zangu zote (Ndani ya CUF) na kama uchaguzi ukifanyika wananchi wa Kinondoni wasifanye makosa wahakikishe wanamchagua Mbunge anayetokana na Chama tawala ili awe kiunganishi kati yao na serikali yao waweze kupata maendeleo kwa haraka zaidi.“amesema
0 comments:
Post a Comment